The Madonna of the Streets
Mary's Rosaries

Home Page

Contact Us

Make a Payment, Methods of Payment, Refund and Exchange Policies

Rosaries
subpages:

How to Pray the Rosary
subpages:

Pictures Main Page
subpages:

Curriculum
subpages:

Website Terms of Use

License Agreement

Sitemap


The Work of God's Children

 Kiswahili Rosary Prayers
This language is also known as Swahili and Kisuaheli.
This language is spoken by 30,000,000 people in Zanzibar, Burundi, Kenya, Mayotte, Mozambique, Oman, Rwanda, Somalia, South Africa, and Uganda.

See also The Work of God's Children page for the illustrated version of prayers in this language.

Rozari Takatifu Ya Kibiblia Ya Bikira Maria Mtakatifu / The Holy Rosary


  Ishara Ya Msalaba / The Sign of the Cross / Signum Crucis
 Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina!

Nakuungamia / Apostles' Creed / Credo
Nakuungamia kwa Mungu baba Mwenyezi,
Muumba wa Mbingu na nchi na Kwa Yesu Kristo mwanaye wa pekee. Aliyezaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa roho mtakatifu. Akateswa kwa mamlaka ya ponsio pilato,Akasulubiwa, akafa, akazikwa na kushukia kuzimu. Siku ya tatu akafufuka katika wafu, akapaa mbinguni, Amekaa kuume kwa baba na atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa roho mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele AMEN.

Baba Yetu / Our Father / Pater Noster
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina.

Another version of
Baba Yetu / Our Father / Pater Noster
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.  Amina.

Doxology
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.

Salamu Maria / Hail Mary / Ave Maria
Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,
mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.

Atukuzwe Baba / Glory Be to the Father / Gloria Patri
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.
Amina.

Kubarikiwe siku zote
Kubarikiwe siku zote kutungwa mimba bila dhambi ya asili kwa Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yetu.

Ee Yesu wangu / Oh, My Jesus
Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

SALAM, MALKIA! / Hail, Holy Queen / Salve Regina
Salam, Malkia! Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam! Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika huku bondeni kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho yako ya huruma, Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu Bikira Maria.

NAMNA YA KUISALI

* Baada ya ishara ya msalaba, tunasali Atukuzwe Baba na zile sala pili za utangulizi, halafu tunalitangaza fumbo; inafuatiwa na Baba yetu (1),Salamu Maria (10) halafu Atukuzwe Baba… na zile sala pili za utangulizi.
Halafu tunatangaza fumbo linalofuata na kuendelea kama ilivyoelezwa hapo juu.
* kwa namna ya pekee wakati wa kusali “Baba yetu” na “Salamu Maria” (10) fanya akili (na moyo!) “kukimbilia” kutafakari juu ya fumbo lililotangazwa.

MAFUMBO YA UUMBAJI

( kwa Jumatatu ) :

  1. YHWH: Mungu Baba kwa njia ya Neno (ΛΟΓΟΣ - VERBUM), [“Awe!”], aumba mbingu na dunia na Roho Mtakatifu ambaye tayari aliutangulia uumbaji kwa hekima yake alikuwa akielea juu ya maji yaliyo kuwa yameufunika uso wote wa nchi akivibariki viumbe.
  2. Mungu amuumba mtu, mwanamme na mwanamke, wote aliwaumba kwa mfano na sura yake.
  3. Mungu amwahidia mwanmke baada ya dhambi ya asili kuwa kwa njia ya uzao wake, Masiha ataponda kichwa cha nyoka – adui wa mwanadamu.
  4. Melkisedeki kuhani mkuu atoa mkate na divai kama sadaka ya shukrani kwa ushindi wa babu mtakatifu Abrahamo (Mwa. 14, 18-20).
  5. Abrahamo aupokea ugeni, atambua na “kumkaribisha” Bwana, Utatu Mtakatifu karibu na mialoni ya Mamre (Mwa. 18, 1-15).
  6. Mungu amweka huru Isaka toka mauti kulingana na ahadi yake (“uzao wako utakuwa mwingi kuliko nyota za mbinguni na kuliko mchanga ulioko pwani ya bahari na kuimiliki miji ya adui zako” – (Mwa. 22, 17) na kuimarisha Agano lake na Abrahamo (“na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia(Mwa. 22, 18)

MAFUMBO YA NGUVU ZA MUNGU

( kwa Jumane ) :

  1. MUNGU, katika nafsi yake, awaokoa watu wake toka utumwani Misri na kuizindua Pasaka ya kwanza ya “umilele” (Kut. 12, 1-15).
  2. MUSA – mfano wa KRISTO - kwa Bakora aigawanya bahari ya Sham kwa ajili ya njia  na uzima wa taifa teule na kuwaangamiza maadui wa Israeli kama isemavyo zaburi ya pili (Zab. 2, 8-9) ya mfalme masiha “uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.”  na kama kisemavyo kitabu cha ufunuo wa Yohana (Ufu. 12, 5) “naye atamzaa mtoto wa kiume atakaye yatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto alichukuliwa mara moja mbele ya Mungu na mbele ya kiti chake cha enzi”.
  3. NGUVU YA MUNGU, katika namna ya wingu ikatulia juu ya sanduku la agano Ambalo lilikuwa limewekwa katikati ya kambi ya wana wa Israeli ambalo katikati Yake kuna tabernakulo takatifu ambamo ndani yake Mungu ana kaa na ambamo taifa teule litapewa ishara tatu zilizokielezo cha Ekaristia Takatifu na Tabernakulo ya Ekaristia Takatifu: Vibao vya Sheria, yaani Neno lake (Verbum), “lililoandikwa kwa kidole cha Mungu” (hivyo kuja kwake moja kwa moja kama Mwana); Bakora ya Musa ni ishara nguvu aliyopewa na Mungu ambayo kwayo Musa aliigawanya ya Sham; Manna iliyoshuka toka mbinguni na ambayo huwashibisha wana wa Israeli huko jangwani.
  4. MUNGU amchagua Daudi na kumpaka mafuta kama Mfalme na Nabii juu ya watu wake Israeli na kuahidi Ufalme Milele kwa mwanae (katika uzao wake).
  5. JUDITA (Jd. 8-16), anayekata kichwa cha mfalme, adui wa wana wateule akiwaweka huru toka utumwani ni mfano wa MARIA aliyevaa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji la nyota kumi na mbili ambayo huseta kichwa cha mfalme wa giza, “nyoka wa kale”, na kuwaweka huru wateule wa Kristo toka utumwa wa yule mwovu.
  6. NGUVU YA ROHO MTAKATIFU inajionyeshe pia Katika ushahidi wa mzee Eleazaro (2 Mak. 6, 18-31), katika watakatifu ndugu wa Makabayo na Mama yao Mtakatifu (2 Mak. 7, 1-41), kwa kutokukubali kuiasi Sheria ya Mungu.

MAFUMBO YA FURAHA / The Joyful Mysteries
( kwa Jumatano ) :

  1. Malaika mkuu Gabrieli ampasha habari Bikira Maria, na kwa “NDIYO” Yake, NAFSI YA PILI YA UTATU MTAKATIFU INAJIMWILISHA KATIKA TUMBO LAKE.
  2. Maria Mtakatifu amtembelea Mtakatifu Elizabeti.
  3. YESU ANAZALIEWA BETLEHEM.
  4. Yesu anatolewa Hekaluni.
  5. Yesu anakutwa Hekaluni.

MAFUMBO YA MWANGA / The Luminous Mysteries
( kwa Alhamisi ) :

  1. Yesu anabatizwa katika mto Jordan na Yohana Mbatizaji. – (Yesu anajipeleka kwa Yohana Mbatizaji ili aweze kubatizwa naye. Yeye habatizwi kwa ajili ya toba bali anapenda “kujishusha” zaidi na kujifanya mdhambi (ila bila dhambi) kati ya wadhambi. Mara baada ya kuingia majini mbingu zinafunguka, Roho Mtakatifu katika umbo la njiwa anatua juu yake na sauti ya Baba inatangaza toka juu mbinguni “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu niliyenipendezwa naye” - Mt. 3, 17).
  2. Yesu anafanya ishara ya kwanza katika maisha yake hadharani katika harusi ya Kana. - (Yesu alikuwa amealikwa pamoja na wanafunzi wake katika harusi ya Kana ya Galilaya. Wakiwa wameishiwa divai Yesu analetewa ombi na mama yake, anabadili maji kuwa divai. Injili inayoeleza tukio hilo inataarifu maneno ya mwisho ya mama Maria akituonya na kutualika daima kwamba «LOLOTE ATAKALOWAAMBIA, FANYENI !» - Yn. 2, 5).
  3. Yesu atangaza ujio wa ufalme wa Mungu. -(Yesu anatangaza kuwa ufalme wa Mbinguni u karibu na kwamba uko tayari kati yetu na kuthibitisha kuwa wataingia humo wale tu walioisafisha mioyo yao na kujinyenyekesha hata kujifanya «wadogo» kama mtoto).
  4. Yesu anabadilika sura katika utukufu wa Mungu juu ya mlima Tabor pamoja na Musa na Elia. - (Yesu anapanda mlima Tabor akiwa pamoja na Pietro, Yakobo na Yohana ili kusali. Mara kwa ghafla anabadilika sura katika utukufu wake wa kimungu anangara kuliko jua, karibu naye wanatokea Musa na Elia wakijadiliana kuhusu utume wake wa kimasiha kwa ajili ya wokovu, kwao yampasa aikabili Yerusalemu. Baba anatualika na anamtolea tena ushuhuda “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye: MSIKILIZENI YEYE” - Lk. 9, 35).
  5. Yesu akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pamoja na Mitume wake katika ukumbi wa mlo wa jioni aliweka Ekaristia Takatifu. - (Juu ya mlima Sion, katika ukumbi wa Chakula cha Jioni, Yesu, akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pa moja na Mitume wake baada ya kuwa amewaosha miguu aliwapa mkate na divai akithibitisha ni mwili wake na damu yake vilivyotolewa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Ni adhimisho la Ekaristia Takatifu). 

MAFUMBO YA UCHUNGU / The Sorrowful Mysteries
( kwa Ijumaa ) :

  1. Yesu asali katika bustani ya Getsemani.
  2. Yesu anapigwa mijeredi.
  3. Yesu anavikwa taji la miiba na anahukumiwa kifo bila hatia.
  4. Yesu anapanda Calvari akibeba Msalaba.
  5. YESU AFA MSALABANI.

MAFUMBO YA UKIMYA WA MUNGU

UKIMYA UNAOFANYA KAZI YA MAPENDO NA YA HURUMA
( kwa Jumamosi ) :

  1. KRISTO, kati ya siku ya kufa na siku ya kufufuka kwake, siku ya “ukimya wa kimungu” aziweka huru roho za wenye haki na kuwaandalia nafasi mbinguni wao pamoja na wenye haki wengine watakao fuata.
  2. MARIA, kwa Upendo ya Kimama na Mama wa Kanisa zima, kwa licha ya Uchungu wa Kalvari, licha ya “upanga” uliompenya Moyo wake pale Kalvari anapata faraja, anatiwa moyo na kukaa siyo tu na Yohana bali hata Pietro na Mitume wengine wakiwa na uchungu, kuchanganyikiwa na usumbufu wa “kashfa” ya Msalaba.
  3. Huruma ya BABA kwa wanadamu haikatizwi na dhambi ya kumwaga damu na kumwua Mwanae-masiha Yesu Kristo, bali anaipokea kama sadaka jumla ya ukombozi wa wanadamu ambao Mungu aliwapenda, akawaumba kwa sura na mfano wake na kwa ajili ya wokovu wao akamtuma Mwanae wa pekee.
  4. MBEGU iliyoanguka chini kwenye udongo ikafa, maisha ya Kristo yaliyo tolewa sadaka na damu yake iliyo mwagika Kalvari vinachipusha leo hii toka katika ukimya wa kimungu maisha mapya na yasiyaharibika kwa wale wanaoupokea kulingana na mapenzi ya moyo wa Kristo.
  5. ROHO MTAKATIFU, katika kimya kikuu cha Jumamosi anaiandaa na kuifinyanga mioyo na akili za wampendao Mungu ili kulipokea tangazo la Ufufuko lisiloweza kuaminika kibinadamu kwa wale wampendao Mungu, kulipokea lisiloaminika (kibinadamu). Kwa tangazo la ufufuko, maana yeye, Yesu Kristo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu: vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu…Yeye ni Mwanzo na Mwisho, mwezayote …Yeye ni Mwana kondoo asiye na hatia milele yote yuko juu ya altare ya mbinguni na yeye tu mwenye kustahili kuchukua kitabu, kuvunja mihuri yake na kukifungua na kumkabidhi Baba kwa utukufu wa milele wa Mungu, wa malaika zake na watakatifu wake”. 

MAFUMBO YA UTUKUFU / The Glorious Mysteries
( kwa Jumapili ) :

  1. YESU ANAFUFUKA.
  2. YESU ANAPAA MBINGUNI.
  3. ROHO MTAKATIFU ANAWASHUKIA MITUME WAKIWA PAMOJA NA BIKIRA MARIA.
  4. Bikira Maria APALIZWA mbinguni.
  5. Bikira Maria AVIKWA TAJI Mbinguni Malkia wa Mbingu na Nchi.
Mtakatifu Mikaeli / Prayer to Saint Michael, the Archangel
Mtakatifu Mikaeli, Malaika Mkuu,

Utulinde katika vita;
Uwe kinga yetu katika maovu na mitego ya Shetani.
Tunakuomba kwa unyenyekevu
Ee Mungu mweke Shetani chini ya mamlaka yako
Nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni,
Kwa nguvu ya Mungu,
Mtupe Shetani motoni
Na Pepo wabaya wote ambao;
Wanazungukazunguka duniani,
Wakitafuta kuangamiza roho za watu. Amina.

Another version of
Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu / Prayer to Saint Michael, the Archangel

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni, kwa nguvu ya Mungu, uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani,ili kuzipoteza roho za watu. Amina.

Usiku wa sifa / Silent Night

Usiku wa sifa
Wa raha na nuru
Alipozaliwa Mwana
Mtakatifu na mwema
Mwana ndiye Mungu
Mwana ndiye Mungu


"God is Love" in Kiswahili is " Mungu ni Upendo. "

 


Creative Commons License
The contents of this webpage are licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
Valid HTML 4.01 Transitional
(this is the bottom of page)